Mwanaume anapaswa kujua mambo yafuatayo kabla hajamfuata mwanamke ambaye hamjui au hawafahamiani njiani kwa njia ya kutaka kuanzisha uhusiano nae
*1.JIAMINI
Mwanaume anapaswa kujiamini na kuacha kujiuliza mara mbilimbili , mbona wakati wa kula chakula watu hawajiulizi mara mbilimbili ujasiri wako ndo utakaofanya kumpata mwanamke yoyote umpendae ndani ya mda muafaka . wakati unamfuata fanya ni kama demu wako na mshazoeana sana na usiogope kukataliwa
*2.ENDELEZA MAZUNGUMZO MAREFU
mwanaume unapomfuata mwanamke hakikisha unaanzisha mazungumzo marefu ambayo yatamfganya mwanamke ajielezee na pia tambua kuwa wanawake wanapenda wanaume wenye stori nzuri
*3.MSIFIE
hakikisha unamsifia mwanamke jinsi alivyovaa , jinsi anavyoongea , mpangilio wa meno yake , rangi ya nguo etc kwa kufanya hivyo itamfanya mwanamke ajisikie mwenye amani mbele yako na apende kuwa karibu na wewe
*4.AHADI ZA KUMJALI
mwanamke ni kiumbe dhaifu hivyo anapendwa kuwa anadeka , mwambie kuwa upo kwa ajili yake na kwamba utamjali na pia fanya kitu chochote (matendo ) kitakacho fanya aamini jambo hili
*5.USIJITAMBE MBELE YA MWANAMKE
Wanawake hawapendi mwanaume mwenye kujisifia kuhusu mafanikio yake ya kiuchumi au hali ya kujionesha kwamba utamhudumia mwanamke , bali hupenda mwanaume yule anaemweka mbele yeye kuliko mali zake tambua kuwa hata uwe mwanaume tajiri duniani ukiwa unajisifia mbelel ya wanawake sio wote utakaowapata
No comments:
Post a Comment